Last Updated on 22/09/25 by Tabibu Fadhili Paulo
Aina za bawasiri
Bawasiri imegawanyika mara 2. Kuna bawasiri ya ndani na bawasiri ya nje
1. Bawasiri ya ndani – Hii ni bawasiri ambayo inajitokeza ndani ya mfereji wa haja kubwa na kwa kawaida mgonjwa anaweza asihisi maumivu yoyote hivyo huwafanya watu wengi kutotambua kuwa wana ugonjwa huu.
Bawasiri ya ndani nayo imegawanyika katika hatua nne tofauti ambazo ni:
Bawasiri ambayo haitoki mahali pake (bawasiri iliyosimama).
Bawasiri ambayo wakati wa haja kubwa inatoka lakini baada ya kumaliza haja kubwa inarudi yenyewe ndani.
Bawasiri ambayo wakati wa haja kubwa inatoka na hairudi tena ndani yenyewe bila kurudishwa na mgonjwa.
Bawasiri inayotoka wakati wa haja kubwa na kubaki nje hata kama mgonjwa atairudisha bado itaendelea kubaki tu nje.
2. Bawasiri ya nje – Hii ni aina ya bawasiri ambayo hutokea eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa. Huwa na kiuvimbe au viuvimbe kadhaa na mara nyingi huambatana na maumivu na muwasho katika sehemu hiyo.
Kwa kawaida mishipa hiyo ya damu (vena) karibu na nje ya tundu la haja kubwa hupasuka na damu huganda.