Bawasiri husababishwa na nini

Last Updated on 22/09/25 by Tabibu Fadhili Paulo

Bawasiri husababishwa na nini?

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ugonjwa wa bawasiri husababishwa na nini.

Bawasiri ni ishara inayokuambia kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kuna kitu hakipo sawa.

Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Huu mfumo ukishakua mbovu unakupelekea kutokupata choo vizuri, unaanza kupata choo kigumu sana wakati mwingine unaweza kukaa siku kadhaa bila kupata choo kabisa.

Mfumo wako dhaifu wa mmeng’enyo wa chakula ndiyo sababu ya chakula kupita bila kumeng’enywa vizuri kwenye utumbo mdogo.

Hivyo chakula kinapitiliza kwenda moja kwa moja kama kilivyo kwenye utumbo mkubwa ambako maji maji ya kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu.

Utakapotaka kupata choo, choo hutokea kikiwa kikavu jambo linalokulazimu kutumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.

Nguvu hii unayoitumia wakati unapata choo ndiyo sababu ya kutanuka kwa misuli na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na pole pole utaanza kuona kinyama kinajitengeneza, na kufuatiwa na maumivu na miwasho kwa ndani, na wakati mwingine unapata kilichoambatana na damu.

Unapoendelea kupata choo kigumu kwa kipindi kirefu misuli nayo huendelea kukwanguliwa na kinyama huongezeka mpaka kinatokea nje na kufanya bawasiri ya nje.

Ukiona unamaliza siku nzima hujapata choo au wakati mwingine inapita siku mbili au tatu au zaidi na hupati choo ni dalili mbaya sana kwa afya yako.

Vyovyote itakavyokuwa hakikisha kila siku unapata choo japo mara moja au mpaka mara tatu lakini isipite siku nzima hujapata choo.

Choo kiwe kilaini na usitumie nguvu nyingi ili kukipata na hata ikitokea choo kilaini sana tuseme unaharisha mara moja au mbili kwa wiki bado ni ishara una afya nzuri.

Choo unachopata kiwe ni kirefu ukubwa wa ndizi na kisiwe kinachokatikakatika kama kile cha mbuzi.

Vitu vifuatavyo vinatajwa kama sababu zinazoweza kukusababishia ugonjwa huu.

Visababishi vya bawasiri:

1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu

2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa

3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile

4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu

5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.

6. Kuharisha sana kwa muda mrefu

7. Kutumia vyoo vya kukaa

8. Kunyanyua vyuma vizito

9. Mfadhaiko unaodumu muda mrefu (stress)

19. Uzito na unene kupita kiasi nk

11. Kutokula matunda kila siku

12. Kutokula mboga nyingi za majani kila siku

13. Kutokunywa maji mengi kila siku

14. Kukaa muda mrefu kwenye kiti

15. Kula ugali wa sembe

16. Kula wali kila siku

17. Kutokula chakula cha kutosha chenye nyuzinyuzi (faiba)

Bawasiri husababishwa na nini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to top