Last Updated on 22/09/25 by Tabibu Fadhili Paulo
Bawasiri ni nini?
Bawasiri ni ugonjwa gani?
Bawasiri au Kikundu au Puru ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa.
Kwa Kiingereza hujulikana kama Hemorrhoid au Piles.
Katika hatua yake ya kuonekana wazi ugonjwa hujitokeza kama uvimbe au vivimbe kadhaa kwenye maeneo ya tundu la haja kubwa.
Karibu katika kila watu wanne mtu mmoja kati yao anasumbuliwa na ugonjwa huu.
Ni ugonjwa wa pili kati ya magonjwa yanayosumbuwa watu wengi zaidi duniani baada ya U.T.I
Kutokana na sehemu au mahali hasa ugonjwa wenyewe unapojitokeza umepelekea watu wengi kuwa na aibu kujisema kwamba wanaumwa ugonjwa huu.
Tatizo la bawasiri linaonekana kuwawapata kirahisi zaidi wanawake kuliko wanaume