Dalili 17 za vidonda vya tumbo

Dalili 17 za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na:

  1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
  2. Kuumwa mgongo au kiuno
  3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu na hamu ya tendo la ndoa.
  4. Kizunguzungu
  5. Kukosa usingizi
  6. Maumivu makali sehemu ya mwili
  7. Maumivu ya Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali
  8. Kichefuchefu
  9. Kiungulia
  10. Tumbo kujaa gesi
  11. Tumbo kuwaka moto
  12. Miguu kuwaka moto na ganzi
  13. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
  14. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
  15. Kukosa hamu ya kula
  16. Kusahahu sahau na
  17. Hasira za mara kwa mara

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.

Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *