Dalili 17 za vidonda vya tumbo
Dalili 17 za vidonda vya tumbo
Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na:
- Kuchoka choka sana bila sababu maalum
- Kuumwa mgongo au kiuno
- Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu na hamu ya tendo la ndoa.
- Kizunguzungu
- Kukosa usingizi
- Maumivu makali sehemu ya mwili
- Maumivu ya Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali
- Kichefuchefu
- Kiungulia
- Tumbo kujaa gesi
- Tumbo kuwaka moto
- Miguu kuwaka moto na ganzi
- Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
- Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
- Kukosa hamu ya kula
- Kusahahu sahau na
- Hasira za mara kwa mara
Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.
Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Utambuzi wa vidonda vya tumbo
Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.
Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.
